Wambura Apinga Maamuzi Yaliyotolewa na Kamati ya Rufaa TFF

Wambura Apinga Maamuzi Yaliyotolewa na Kamati ya Rufaa TFF
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)  Michael Richard Wambura amesema hajakubaliana na maamuzi yaliyochukuliwa na kamati ya rufaa ya maadili ambayo imetupilia mbali rufaa yake hapo jana.


Akiongea leo na wanahabari, Wambura amesema kuwa kamati iliyopitia rufaa yake na kutoa maamuzi jana haina uhalali na wala sio huru hivyo maamuzi yake yameegemea kulinda maslahi ya upande wa walalamikiwa ambao ni TFF.

Aidha Wambura amesema kamati hiyo haijatoa haki ya kumsikiliza mlalamikaji badala yake kamati imesimama kama chombo cha kupitia malalamiko kisha kumtetea mlalamikiwa hivyo anaamini majibu yaliyotolewa hayana mtazamo wa kamati huru.

Kamati hiyo jana ilitangaza kutobadili maamuzi ya kamati ya nidhamu ambayo yalitolewa Machi 15 ya kumfungia Wambura kutojihusisha na soka maisha, adhabu ambayo imekuwa ikipingwa na Wambura mara kwa mara.

Makosa matatu ambayo yamesababisha kufungiwa maisha kwa Wambura ni kupokea fedha za shirikisho malipo yasiyo halali, kugushi barua na kushusha hadhi ya Shirikisho.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad