Wamiliki wa Sober Houses Wajibu Tuhuma za Serikali

Wamiliki wa Sober Houses Wajibu Tuhuma za Serikali
Wamiliki wa nyumba zinazosaidia waathirika wa dawa za kulevya nchini yaani 'Sober Houses' wamekanusha tuhuma za serikali kwamba wanatumia nyumba hizo kwa maslahi binafsi


Akiongea na waandishi wa habari Jiji Dar es Salaam Katibu wa Umoja wa Wamiliki wa Sober Houses, Pili Missanah, amekanusha vikali tuhuma zilizotolewa na baadhi ya Wabunge mnamo April 25, 2018 kwamba baadhi ya wamiliki wa nyumba hizo huwachoma sindano za dawa za kulevya baadhi ya waathirika pindi wanapokaribia kupona ili wazazi au walezi waendelee kuchangia fedha kwenye nyumba hizo.

Aidha, Pili Missanah amesema kwamba wapo tayari kutoa ushirikiano na pia wameiomba serikali kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kufanya uchunguzi na kwamba, hawajapata malalamiko yoyote kutoka kwa wazazi au walezi wa waathirika hao kuhusu ya tuhuma hizo.

Pili amesisitizia kuwa kuna nyumba 22 pekee Tanzania na hadi sasa zina waathirika 737 wanaopatiwa matibabu wakiwemo wanawake 21 na wanaume 726 na wamefanikiwa kuokoa watu zaidi ya 4,000 ambao wameachana na matumizi ya dawa za kulevya na wanaendelea na shughuli nyingine za kimaendeleo.

Top Post Ad

Below Post Ad