" Wasanii wa Bongo Fleva msidanganywe na uwingi wa Folowazi Mitandaoni ", Ommy Dimpoz

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Msanii maarufu wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz amewataka Wasanii wenzake kuacha tabia ya kuamini na kudhani kuwa wale Watu wote ( Followers ) wanaowafuatilia katika Mitandao yao ya Kijamii huwa ni kweli wapo nao karibu na wanawaunga mkono katika Kazi.

Msanii huyo alieleza Kisa kimoja ambacho anasema hatokuja kukisahau maishani mwake pale ambapo alikuwa akienda kufanya ' show ' yake Mkoani Mtwara hivyo kama kawaida yake akawatangazia ' Folowazi ' wake katika mitandao yake ya Kijamii na kuwataka waende wakamuunge mkono kwa kuingia kwa wingi.

Ommy Dimpoz amesema kwamba mara baada tu ya kutoa tangazo hilo alipata majibu mengi sana katika ' Kurasa ' zake za Mitandao huku wengi wa ' Folowazi ' wake wakimuhakikishia kabisa kwamba watajumuika nae Mkoani Mtwara na Yeye ( Ommy ) akawa tayari ameshapiga Hesabu zake za kimoyomoyo kwamba kwa ' mrejesho ' ule wa majibu ya ' Folowazi ' wake basi umasikini wake ungeishia pale Mkoani Mtwara.

Cha ajabu na kusikitisha Ommy Dimpoz anasema siku ya ' show ' yake hiyo pale Mkoani Mtwara Watu walioingia ukumbini hawakuzidi hata 70 lakini ambao walimuhakikishia kuja walikuwa kama 3000 hivi katika Mitandao yake yote ya Kijamii ambayo yupo kila siku.

Baada ya kuona vile Ommy Dimpoz anasema alirudi katika Kurasa zake za Kijamii na kukagua wale ' Folowazi ' wake wote waliomuhakikishia kwenda katika ' show ' yake ndipo alipochoka kwani wengi wao kumbe walikuwa hawatoki Mtwara na walikuwa mbali mno Kijiografia.

Kilichomkera zaidi Ommy Dimpoz anasema kuna ' Folowa ' wake mmoja anakumbuka alipoweka tu Tangazo lake kwamba atafanya ' show ' Mtwara yule ' Folowa ' pale pale akamjibu hivi namnukuu..." Usijali mwana Ijumaa natia maguu katika Show yako tena mapema sana na nitaingia na tiketi yangu ya VIP kwani nakukubali kuliko maelezo na hapa sasa naandaa Nguo ya kuvaa siku hiyo ili tujumuike pamoja na nisipotokea basi najikata Uume wangu mbele yako ".

Ndipo Ommy Dimpoz baada ya ile siku ya ' show ' yake kupita akaingia tena Mtandaoni na kumfuatilia huyu ' Folowa ' wake ambaye alimuhakikishia kabisa kuwa angehudhuria siku ile aliyoposti alikuwa wapi ndipo akagundua kwamba kumbe Jamaa ( Folowa ) yule aliyekuwa na ' majigambo ' yote yale aliposti akiwa Kijiji kimoja hivi cha Kyaka Nkunde kilichopo Mkoani Kagera na wala kumbe hakuwa pale Mkoani Mtwara wala Mikoa ya karibu ndipo toka siku hiyo akasema hajawahi tena na hatokuja kuwaamini tena kwa 100% ' Folowazi ' wake.

Nadhani hili litakuwa ni fundisho kama siyo funzo kwa wengine.

Nawasilisha.

Top Post Ad

Below Post Ad