Kutoka nchini Indonesia, watoto wawili, mvulana akiwa na miaka 15 na msichana miaka 14 jana April 24, 2018 wamefunga ndoa baada ya kupewa ruhusa kisheria kufanya hivyo.
Inaelezwa kuwa watoto hao walikwenda kutafuta ruhusa kwenye mahakama ya kidini ambapo inaelezwa kuwa serikali huwa haitoi ruhusa ya watoto kuoana mpaka mahakama ya kidini itoe ruhusa.
Kesi ya watoto hiyo imekabiliwa na upinzani mkubwa ndani na nje ya nchi hiyo huku serikali ikipanga kufanya mabadiliko ya sheria.
Indonesia ni nchi yenye idadi kubwa ya Waislamu na wasichana wake wengi wadogo wameolewa.
Sheria ya nchi hiyo kuhusu ndoa ni kwamba, msichana kuanzia miaka 16 na mvulana miaka 19 na kuendelea wanaweza kuoana lakini wanaweza kuoana hata chini ya umri huo kama mahakama ya kidini itaidhinisha.