Mahakama ya kijeshi huko Misri imewahukumu watu thelathini na sita adhabu ya kifo kutokana na makosa ya mashambulizi dhidi ya makanisa ya Coptic.
Watu sabini walikufa kutokana na shambulizi la bomu katika kanisa kuu la ki Coptic mjini Cairo mwishoni mwa mwaka 2016, na makanisa ya Alexandria na Tanta yaliripuliwa siku kama hiyo mwezi wa nne mwaka uliofuata.
Tayari kundi la wanamgambo wa kiislamu wenye msiamamo mkali wamekiri kuhusika na mashambulizi hayo matatu. Wameendelea kukiri kuwa kazi yao kubwa ilikuwa kuwashambulia wakristo wachache, pamoja na mamlaka ya kijeshi.
Misri inahitaji mahakama kupeleka kesi za namna hiyo kwa Mufti mkuu nchini humo kwa kuzingatia adhabu ya kifo kabla ya hukumu ya mwisho.