Watu 57 Wameuawa kwa Bomu Katika Kituo cha Kujisajili

57 wauawa kwa bomu katika kituo cha kujisajili
Watu 57 wamuawa katika shambulio la bomu la kujitoa muhanga lililolenga kituo cha kuandikishia wapiga kura katika mji mkuu Kabul nchini Afghanstan.
Taarifa kutoka mamlaka mjini Kabul zinasema kuwa kati ya watu hao waliouawa kutokana shambulio wakiwa katika mistari ya kujiandikisha kati yao wamo wamo wanawake 21 na watoto watano,huku wengine 119 wakijeruhiwa pia.
Kundi la kigaidi la Islamic State (IS) wamesema kuwa wao ndiyo wanaohusika na shambulio.
Kazi ya uandikishaji wapiga kura nchini humo imeanza mwezi uliopita ikiwa ni maandalizi kwaajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Taarifa kutoka ndani ya IS zinasema kuwa mtu aliyetekeleza shambulio hilo alikuwa amevalia mkanda wa vilipuzi na alikilenga kituo cha kujiandikishia cha eneo la Dashte Barchi magharibi mwa Kabul.

Dashte Barchi eneo lenye idadi kubwa Waislam wa Kishia ambao wamekuwa wakilengwa na kundi la kigaidi la IS.
Watoto waliouawa katika shambulio hilo,walikuwa wamesimama pia katika mistari ya watu waliokuwa wanajiandikisha jumapili asubuhi.

Mlipuko huo pamoja na kusababisha vifo lakini pia umeharibu magari magari.Hadi sasa kumekuwa na mashambulio manne tangu kuanza uandikishaji huo wiki iliyopita.
There have already been at least four attacks on such centres since voter registration got under way a week ago.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad