Waziri Mwigulu Aagiza Kukamatwa kwa Madereva Wanaosababisha Ajali

Waziri Mwigulu Aagiza Kukamatwa kwa Madereva Wanaosababisha Ajali
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi kuwaweka ndani madereva wanaosababisha ajali kutokana na mwendo kasi na baadaye kupelekwa Mahakamani.



Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akijibu muongozo wa Mbunge wa Ulanga Morogoro Mhe. Goodluck Mlinga, juu ya chanzo cha ajali ya basi la City Boy kutoka Karagwe Mkoani Bukoba kuelekea Dar es Salaam ambalo liligongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lililokuwa linatoka Singida kuelekea Igunga usiku wa Aprili 04 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 12.

“Hatuwezi kuacha watu wanapotea kwa ajili ya uzembe wa mtu mmoja na kuleta hasara na vilio vikubwa kwa Watanzania,” alisema Dkt. Mwigulu.

Amesema, ajali nyingi zinazotokea hapa nchini zinasabishwa na mwendokasi na sio tatizo la miundombinu ambapo katika ajali zilizoripotiwa ajali 1500 zilisababishwa na mwendo kasi na ajali 89 zimetokana na miundombinu.
Aidha Dkt. Mwigulu amesema, Tanzania ni moja ya nchi zenye barabara bora hivyo ajali nyingi zinazotokea husababishwa na uzembe wa madereva pamoja na mwendokasi.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mr mwigulu Nchemba, majibu na actions zako juu ya mauaji ya ajali nayaona simplistic mno. Yana mapungufu na hayajalenga kuzuia utokeaji wa ajali Tanzania. Dereva kuksmatwa pekee kamwe haitoshi na haizuii kutokea ajali. Naona umelitazama tatizo kupitia the individualistic perspective. Una hakika chanzo ni uzembe pekee? Zipo sababu nyingi nyuma yake, ikiwemo uchovu, stress, kulundikiwa kazi, ujuzi mdogo, na nature ya ajira yake nk. Tafadhali lichukulie tatizo hili kama emergency na enough is enough. Km ilivyo kwa makinikia, Tafadhali unda tume inayowaleta multi sectors pamoja, kwa wizara au taasisi moja pekee haitaweza tatua tatizo hili. Ita wasomi waliobobea na mfanye analysis ya tatizo hili kwa nia ya kulitokomeza. Sasa akamatwe Dereva pekee, bila company iliyomwajiri? Kuliko kutumia hiyo responsive action pekee inabidi utengeneze pro-active intervention, kwani ni hiyo tu itapunguza ajali. Miaka yote madereva wakifsnya ajali wanakamatwa (ambayo ni saw a) lakini je hajali mbona hazijapungua? Hii ni evidence kwamba hiyo technique pekee, bado haina nguvu na pengine si sustainable. Hili kulitatua, itahusu iliyojengwa na wengi wakiwemo wewe mwenyewe, police, justice, wizara ya ujenzi, wanaoregista biashara ya usafiri na madereva wapya, bunge, na wengine. Miundo mbinu ingawa tumejitahidi, lakini bado (lakini hilo linaweza kuwa katika long term plans) ila intervention ya haraka ni lazima kwa ujumbe. Enough is enough

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad