Wema Sepetu Ampa Ahadi Nzito RC Makonda " Nakuahidi Sitokuangusha"

Wema Sepetu Ampa Ahadi Nzito RC Makonda " Nakuahidi Sitokuangusha"
Baada ya kuibuka mshindi wa tuzo mbili za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF), Wema Sepetu amemuhaidi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutomuangusha katika suala zima la uigizaji.

Muigizaji huyo amemshukurua RC Makonda kwa kumtia moyo kwani ni kitu ambacho anakihitaji sana kwa kipindi hiki.

“Lakini pia naomba nikuahidi, sitokuangusha maana kumuangusha RC wako nako sio pambe kabisa,” amesema Wema.

Kauli ya Wema inakuja mara baada ya RC Makonda kumtaka muigizaji huyo kuweka picha ya tuzo aliyoshinda katika ukurasa wake wa Instagram baada ya baadhi ya watu kujitokeza na kukosoa tuzo hizo.

“Picha ya hapo juu uliyoomba ni mmiliki halali wa Filamu ya Heaven Sent ambaye kajisajili Cosota na Bodi ya Filamu, anazo haki miliki zake zote na ndio aliyeshinda Best Actress 2018 kwa kuwa amekidhi sababu zote za kuwa Mshindi,” amesema.

Wema ameendelea kwa kusema anataka tasnia ya Filamu iwe na watu wenye kujielewa na wenye upeo mkubwa, sio wenye kukurupuka na kuvamia jambo bila kudadavua na kujua ni kitu gani kinatakiwa kufanyika.

“Yote yanawezekana, wasanii ni watu wenye wadhifa mkubwa sana, najivunia kuwa mmoja kati yao. Ninajua hata wewe unajivunia kuwa kati yetu sisi ukiwa kama Mlezi ukituongoza kila leo kutaka tufike sehemu nzuri na Inshallah tutafika,” ameeleza Wema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad