Werrason Akubali Uwezo wa Christiani Bella Amuahidi Kufanya Naye Kazi

Werrason Akubali Uwezo wa Christiani Bella Amuahidi Kufanya Naye KaziMsanii Supersatar wa Congo Noël Ngiama Makanda alimaarufu kama Werrason amekubali kufanya kazi na msanii wa muziki wa bongo fleva Christian Bella baada ya kumkubali kutokana na uwezo wake na kazi zake.


Werrason amesema hayo alipokutana na msanii Christian Bella na kuonyesha hisia zake juu ya msanii huyo jambo ambalo Christian Bella ameliona ni jambo kubwa sana katika muziki wake kuona watu ambao alikuwa akiwasikiliza toka wakiwa wadogo saizi wanakubali kazi zake na kukubali kufanya kazi pamoja na yeye.

"Imethibitishwa sasa nitafanya kazi na Werrason  the king of jungle, nadhani kujituma juhudi zangu na kutokata tamaa leo hii ma Star Wakubwa ambao nilikua nawashangaa kwenye TV nikiwa mdogo kutoka DRC wananipa heshima na kunikubali. Nasema Asante Mungu Asante pia sana Kwa watanzania kwa kunipa na fasi na kunikubali na kuni support leo hii miaka 13 kwenye game bado naonekana mpya" alisema Christian Bella

Christian Bella kwa sasa anatamba na wimbo wake 'Niende wapi' ambao amemshirikisha rapa Joh Makini kutoka katika kampuni ya Weusi. Itazame hapa kazi yake mpya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad