Wimbo wa Leka Dutigite wa Kigoma All Star ni Wangu si wa Kund- Linex

Wimbo wa Leka Dutigite wa Kigoma All Star ni Wangu si wa Kund- Linex
Msanii Linex amesema wimbo ‘Leka Dutigite’ ulioimbwa na kundi la Kigoma All Star ulikuwa wa kwake.

Muimbaji huyo ameiambia TV E kuwa aliuandika wimbo huo kwa asilimia 90 ndipo akawapa wengine waimbe kwa sababu wengi wao walikuwa hawajui mitaa ya Kigoma.

“Kigoma wimbo sio wa kundi ni wa kwangu mimi nikaamua kuwapa watu, tufanye wote,” amesema Linex.

“Kwa hiyo ule ni wimbo wangu na asilimia kubwa ya ule wimbo mimi ndio nimechora kwa sababu asilimia kubwa ya watu ambao walikuwa wameimba kwenye ule wimbo walikuwa hawajui ule mtaa ukoje zaidi ya Baba Levo na Chege,” amesisitiza.

Wimbo huo ulikutanisha wasanii kama Abdu kiba, Baba Levo, Banana Zorro, Chege, Diamond plantimuz, kigoma all stars, Leka Dutigite, Linex, Makomando, Mwasiti, Ommy dimpoz, Queen Darling na Rachel,
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad