Winnie Mandela Kuzikwa April 14 kwa Heshima Zote za Serikali

Winnie Mandela Kuzikwa April 14 kwa Heshima Zote za Serikali
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametoa taarifa rasmi juu ya mazishi ya Winnie Mandela ambaye Taifa hilo linamtambua kama mama wa Taifa, aliyefariki April 1, mwaka huu.


Akizungumza mara baada ya kuwasili nyumbani kwa familia ya marehemu, Rais Ramaphosa amesema Winnie Mandela atazikwa kwa heshima zote za serikali na utamaduni wa Afrika Kusini hapo April 14, huku zikitanguliwa na shughuli zingine za mazishi kuanzia April 11.

Rais Ramaphosa ameendelea kwa kusema kwamba kama Taifa linatambua mchango wa Winnie Mandela, hivyo watampa heshima zote pamoja na watu wote wanaowatakia mema taifa la Afrika Kusini.

“Kwa ngazi ya serikali ya kitaifa, tumetangaza kuwa Winnie Mandela atakuwa na mazishi ya kitaifa rasmi. Tungependa kutoa shukrani zetu na shukrani zetu kwa wengi nchini kote na ulimwengu ambao wanatutaka sisi vizuri, "amesema Rais Ramaphosa.

Winnie Mandela alikuwa mke wa pili wa aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, na alikuwa ni mmoja wa wapigania uhuru wa watu weusi na kuendeleza harakati hata wakati viongozi wa ANC akiwemo Nelson Mandela wakiwa wamefungwa jela, kwa muda wa miaka 27.



Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Vipi hizi sare za ANC? Zina uhusiano wowote na na sare za CCM?

    ReplyDelete
  2. Ila alikuwa mrembo. Niliwahi kusoma makala fulani iliyoandikwa na aliyekuwa bwana jela kaburu lakini baadaye wakawa narafiki sana na Madiba. Anasema bila kudhani (sheria ilikuwa hairuhusu watoto kutembelea gereza la roben) winnie alipokuja kumwona Mandela, bwana jela alishtukia winnie akitoa kitoto kichanga-kijukuu chao ambacho alikificha ndani ya blanket alilojifunika kwaajili ya baridi kali. Inashangaza aliweza kupita na mtoto katika geti kuu lenye ulinzi wa hali ya juu bila kushtukiwa. Alitaka mumewe akione kijukuu chao.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad