Yaani Siku Davina Akiolewa Tena Naandamana- Maya

MWIGIZAJI mkongwe Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa, siku mwigizaji mwenzake, Halima Yahya ‘Davina’ akiolewa tena, ataandamana. Akichonga na Za Motomoto News, Maya alisema kuwa, Davina ambaye ni rafiki yake wa kuzikana tayari amezaa watoto watatu na baba wawili tofauti na ameumizwa mno na mapenzi hivyo hataki kusikia akiolewa tena na ikitokea ataandamana.

“Yaani siku Davina akiolewa tena naandamana maana wanaume wamemtenda sana jamani, kwa sasa ni wakati wa kutafuta pesa tu kwa kufanya biashara mbalimbali kama ambavyo anafanya ili kuweza kuwalea watoto wake,” alisema Maya. Alipoulizwa Davina alisema kuwa, ni kweli ameumizwa mno na mapenzi hivyo kwa sasa anachofikiria ni kutafuta pesa zaidi ndiyo maana amekuwa akisafiri nje ya nchi kuchukua bidhaa za biashara ili aweze kuendesha maisha yake na wanaye.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad