Siku moja baada ya kuwasili nchini wakitokea Ethipia kwenye mchezo wa kombe la shirikisho la CAF dhidi ya Welayta Dicha,mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga, wanakwea ‘pipa’ kesho mchana kulekea jijini Mbeya tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya wenyeji Mbeya City uliopangwa kuchezwa jumapili kwenye uwanja wa Sokoine.
Kaimu kocha mkuu Noel Mwandilla amesema kuwa hali ya kikosi chake si mbaya licha ya safari na mchezo mgumu wa kombe la shirikisho na wako tayari kwa ajili ya kupambana kuhakikisha timu inapata pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo wa ugenini.
Watu wote wanafahamu kazi ngumu tuliyifanya juzi kule Ethiopia,tuko sawa na tayari kwa mchezo wa jumapili, mpira wa miguu unatuongoza kuwa tayari kwa mapambano muda wowote, nia yetu ni kushinda na kupata poiti tatu muhimu ambazo zitatusongeza zaidi kwenye mbio za ubingwa, amesema Mwandilla.
Kwa upande wake daktari wa kikosi cha Yanga, kiungo Papy Kambamba hatakuwa sehemu ya mchezo huo wa jumapili, kupisha majeraha ya mguu wa kulia aliyopata kwenye mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Welayta Dicha,huku mshambuliaji Ibrahim Ajib akitarajia kurejea rasmi kikosi baada ya kupona Maralia.
Papy hatakuwepo, aliumia Ethiopia, tukiwa kule tulimpatia matibabu ya awali,kesho atakuwa hospital kwa vipimo zaidi, Ibrahim Ajib atarejea kikosini kwa sababu amepona Maralia,kuhusu Andrew Vicent hakuna shaka juu yake yuko vizuri anaweza kucheza ila itategema na waalimu kama wataona inafaa, alisema Dr Bavu.
Yanga imefuzu hatua ya makundi baada ya kufanikiwa kuitoa Welayta Dicha kwa ushindi wa jumla wa magoli 2-1.