Yanga yadondokea timu za Africa Mashariki

Klabu ya soka ya Yanga imepangwa na timu mbili kutoka nchi za Africa Mashariki kwenye kundi D, la michuano ya Kombe la Shirikisho barani Africa, kwenye droo iliyochezeshwa jijini Cairo leo mchana.

Yanga imepangwa na timu za Rayon Sports kutoka Rwanda ambayo katika hatua ya mtoano imewatoa mabingwa wa Africa mwaka 2016 Mamelodi Sondowns ya Africa Kusini.

Pia katika kundi hilo kuna timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya ambayo nayo imetinga katika hatua ya makundi baada ya kuitoa Supersports United pia ya Africa Kusini. Gor Mahia pia iliibuka bingwa wa michuano ya Sportpesa msimu uliopita.

Timu ya nne katika kundi hilo ni U.S.M Alger ambayo inatokea nchini Algeria ikiwa imefuzu hatua ya makundi kwa kuitoa Maniema Union ya DR Congo.

Yanga yenyewe imetinga hatua ya Makundi baada ya kuitoa Wolayta Dicha ya Ethiopia kwa jumla ya ushindi wa mabao 2-1. Mechi za hatua ya makundi zinatarajiwa kuanza Mei 4 na 6.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad