Yanga Yawatahadharisha Simba " Msibweteke Mechi ya Jpili"

Yanga Yawatahadharisha Simba " Msibweteke  Mechi ya Jpili"
Makamu Mwenyekiti wa Tawi la Umoja la Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Waziri Jitu amedai timu yake kushindwa kupata alama tatu kwa baadhi ya michezo waliyocheza kuwa Simba isijipe imani kwamba itaweza kuwafunga.


Waziri Jitu ametoa kauli hiyo zikiwa zimesalia takribani siku 4 kuelekea mpambano wa jadi ambao unatolewa macho na kila mpenda soka nchini kujua ni nani atakuwa mshindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili Aprili 29, 2018.

"Yanga kushindwa kuchukua pointi tatu kwa baadhi ya michezo Simba isijipe imani kwamba inaweza ikatufunga, mimi nitakupa mfano hai, mzunguko wa kwanza ilikuwa hivyo hivyo walikuwa wanasema Yanga mbovu. Simba imefanya usajili wa Bilioni 1.5 lakini hatima yake dakika 90 ndio zimemaliza mchezo, tumekwenda patapata yaani moja moja, siku zote katika historia ya Simba na Yanga ni kwamba mwenye timu nzuri ndio huwa anapata adhabu na wasimba wa zamani wanalijua hili", amesema Waziri.

Pamoja na hayo, Waziri ameendelea kwa kusema "sasa mimi niwaombe Simba wasibweteke mechi ya Jumapili. Yanga yupo vizuri na asipige hesabu kwamba anaenda kumfunga Yanga mpira dakika 90, Yanga anaenda kumpiga Simba Jumapili".

Kwa upande mwiingine, Waziri amesema anaamini kabisa kuwa hamasa waliyopata wachezaji kuelekea katika mchezo huo na michezo iliyobakia ya Ligi inatosha kuonyesha kiwango chao katika mchezo wao dhidi ya mahasimu na wanaamini wachezaji wote hawatakubali kufungwa na Simba.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad