Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe amedai serikali kuwa inapanaga kutekeleza miradi mikubwa ili hali haina pesa ya kutekeleza miradi hiyo ambayo ameielezea kuwa ni gharama kubwa.
Akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Zitto amesema kuwa licha ya kujigamba kuwa serikali ina uwezo wa kujenga mradi huo lakini ukweli ni kwamba haina pesa ya kufanya miradi hiyo.
Awali akitolea ufafanuzi suala hilo waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya makazi William Lukuvi alisema, suala la ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa stiglers linamanufaa makubwa kwa taifa.
Zitto Kabwe Aichana Serikali " Ukweli ni Kwamba Hamna Pesa"
2
April 18, 2018
Tags
Kwa hivyo furaha yake yeye Zito Kabwe ni kuona serikali inashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo? Kama kweli serikali haina pesa ya kutekeleza miradi hiyo lakini inapambana kuhakikisha ianafanya kitu kizuri kwa ajili ya Tanzania na watanzania basi kama wazalendo wa nchi hii tunapaswa kujivunia sana na Serikali yetu. Na kama serikali yetu itaendelea na mwendo huu huu wa kasi ya kuhakikisha nchi yetu inajitekelezea miradi yake wenyewe kwa uwezo tulionao bila ya kukimbilia kuomba misaada kutoka kwa serikali za kigeni basi watanzania tunapaswa kujivunia na Serikali yetu. Kauli ya Zito Kabwe ni maneno ya kulishwa kutoka kwa nchi mabeberu zisizozitakia mema nchi za Africa na Zito ni miongoni mwa vibaraka wa hovyo kabisa kuwamo ndni ya jamii ya watanzania.
ReplyDeleteKm Serikali haina pesa nilifikiri mtanzania halisi angesema 'hatuna pesa' na si 'hamna pesa' kwani zito wewe si mtanzania?
ReplyDelete