Zitto Kabwe Alifikisha Sakata la Abduli Nondo kwa Wazee wa Kigoma “Wazee wa Ujiji Sasa Mkae Tumalize Haya Mambo ya Kipuuzi”

Zitto Kabwe Alifikisha Sakata la Abduli Nondo kwa Wazee wa Kigoma “Wazee wa Ujiji Sasa Mkae Tumalize Haya Mambo ya Kipuuzi”
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na kuonyesha kuchoshwa na baadhi ya mambo ambayo yanaendelea nchini na kuamua kuwaomba wazee wa Ujiji Kigoma wakae ili kuweza kumaliza mambo hayo anayodai ni ya kipuuzi.


Zitto Kabwe amesema hayo baada ya Idara ya Uhamiaji kumuhoji kuhusu uraia wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania, Abdul Nondo jambo ambalo Zitto Kabwe anasema idara ya uhamiaji inatumika kisiasa dhidi ya mwanafunzi huyo.

"Sio kosa hata kidogo Abdul kuzaliwa Ujiji Kigoma. Imekuwa tabia ya Serikali kuwapa kesi za uraia watu wanaotoka mikoa ya magharibi hasa Kigoma. Suala la Nondo ni vita dhidi ya Watu wa Kigoma. Tutapambana. Tutampigania Abdul Nondo. Watanzania tusikubali upuuzi huu wa watu wa Uhamiaji kuwafanya raia wa mikoa kama Kigoma kuwa raia wa daraja B" alisema Zitto Kabwe

Aidha Zitto Kabwe alikwenda mbali na kusema kuwa mwanafunzi huyo ni mjukuu wa moja ya muasisi wa TANU ambaye pia alipigania uhuru wa Tanganyika

"Abdul Nondo Abdul Omar Mitumba, mjukuu wa Marehemu Mzee Omar Mitumba, mwasisi wa TANU na mpigania Uhuru wa Tanganyika leo anaitwa na maafisa Uhamiaji eti kuhojiwa uraia. Hao maofisa uhamiaji na aliyewatuma hawana 'credentials' ambazo Babu yake Nondo, Mwenyekiti wa TSNP anazo. Wazee wa Ujiji sasa mkae. Tumalize haya mambo ya kipuuzi" alisisitiza Zitto Kabwe

Mwanafunzi Abdul Nondo aliitwa leo idara ya uhamiaji kuhojiwa juu ya uraia wake na kujaza fomu hivyo anapaswa kufika tena ofisi za uhamiaji tarehe 20 mwezi huu kwa ajili ya kupeleka vyeti vya kuzaliwa yeye, baba na mama yake, na bibi na babu kwa pande zote mbili za wazazi wake.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hata yeye Zito Kabwe inafaa kuchunguzwa uraia wake kwani hakuna Mtanzania halisi mwenye hulka za hovyo za kisiasa kama yeue. Zito anamamlaka gani ya kisheria yakwenda kuingilia au kuzuia utendaji halali wa kazi wa kisheria na kikatiba wa Taasisi nyeti kama ya uhamiaji? Yeye Zito Kabwe hana macho lakini hata kusikia hasikii? Hajasikia yakwamba Mwanasheria maarufu kule Kenya kaondoshwa kenya kwa tatizo la uhamiaji? Zito amekuwa mtu wa fitna na kutaka kuona Tanzania ikikatika vipande vipande kimajimbo,kikabila na kitaifa kwani hata kule Zanzibar amekuwa ni miongoni wa watu wenye kuwajaza fitna wazanzibari kula kukicha.Kimataifa Zito amekuwa miongoni mwa mafitina wakubwa kabisa wanaopeleka fitna jumuia za kimataifa katika kushawishi kuwekea vikwazo vya misaada vya kimaendeleo Tanzania. Na Kwa kitendo chake hiki cha wazi cha kukampeni juu ya ujimbo katika suala hili la Abduli Nondo inaonesha dhahiri kuwa Zito ni Mkabila. Ni aibu na mambo ya hovyo suala la kitaifa Zito kwenda kulifanya ajenda ya kikabila. Tukisema humu mitandaoni kuhusiana jinsi gani wanasiasa ya aina wa akina Zito ni Janga kwa Taifa watu wanaona labda porojo za mitandaoni lakini nchi kama Tanzania yenye makabila zaidi ya mia moja na zaidi 100 na kutu ni hatari kuwalea wanasiasa wanaotafuta umaarufu katika misingi ya kikabila na ujimbo kama Zito. Hata Baraka Obama kule Marekani watu wa chama cha tawala Republicans walihoji kuhusiana na uraia wake na hawakuwahi kutokea wanasiasa au mwanasiasa kutoka kule nyumbani kwao Hawaii alipozaliwa Obama kuleta mambo ya kipuuzi ya kuanza kukampeni ujimbo ingawa Hawaii kiuhalisia ni visiwa venye hadhi yakuwa nchi tofauti kabisa katika Muungano wa majimbo ya Marekani. Alichokifanya Obama ni kuwakilisha nyaraka zake halisia katika mamlaka husika na kukata mzizi wa fitina juu ya uraia wake. Sasa leo kwetu utaona Zito Kabwe anaendesha kampeni ya kuipaka matope Taasisi husika inayohusika na masuala ya uhamiaji ishindwe kufanya kazi yake kwa kuanzisha Kampeni za kikabila? Zito inabidi wakati mwengine afikiri katika matendo yake kabla hajakurupuka kwani katika kukurupuka kwake huko iko siku ataangukia pabaya na asije akasingizia kuonewa kwani maonevu anayatafuta kwa nguvu zake zote.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad