Zitto Kabwe amjibu Polepole " Ninajua Ninachokisema Msizani Watanzania Mandondocha"

Zitto Kabwe amjibu Polepole " Ninajua Ninachokisema Msizani Watanzania Mandondocha"
Baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole kumtuhumu Mhe. Zitto Kabwe kupotosha taarifa za CAG kuhusu kupotea kwa shilingi trilioni 1.5, kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo ameibuka na kujibu mapigo.



Zitto ametumia mtandao wa Twitter kujibu tuhuma hizo za Polepole kwa kumwambia amekuwa Mwenyekiti wa PAC/POAC kwa miaka nane hivyo anafahamu kile anachokisema.

“Serikali ya CCM ilidhani Watanzania ni mandondocha,wanapelekwa pelekwa tu. Nimekuwa Mwenyekiti wa PAC/POAC kwa miaka 8. Ninajua ninachosema.” ameandika Zitto.

“Jumla ya TZS trilioni 1.5 hazina maelezo ya matumizi yake Katika mwaka 2016/17. Sitajibishana na Mwenezi wa CCM, yeye size yake @AdoShaibu,” ameongeza.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Zito lazima awe muanagalifu na siasa anazoziendesha zitamfikisha pabaya. Kama anasema watanzania si mandonsosha ana maana gani? Yeye kwa mawazo yake anafikiri serikali ya Magufuli ni serikali ya kihuni kiasi cha kuwadanganya Watanzania? Huyo mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ni miongoni mwa watumishi wa serikali ya Magufuli angeweza tu kumuamrisha kutoa taarifa za hesabu za serikali zenye kuifeva serikali lakini utaona jinsi gani ilivyompa uhuru wa kufanya kazi zake katika hali ya uwazi kabisa kama watanzania tunapaswa kumpongeza sana muheshimiwa raisi na serikali yake kwa kufanya kazi kwa uwazi kabisa. Ni serikali na viongozi wachache duniani wanaoweza kuruhusu au kuwaruhusu watumishi wanaowaongoza kuinyoshea kidole serikali inayowaongoza kwa manufaa ya Umma. Hata kama kunaupotevu au kasoro katika mahesabu basi ni Mpumbavu tu peke yake ndie anaeweza kusema Magufuli na serikali yake wameiba pesa. Wazungu wa Makinikia ya mchanga wa dhahabu walikuwa wapo tayari kumpa Magufuli na baadhi ya Watumishi wake kiasi chochote cha pesa wanachokihitaji ili wazungu wale waendelee kutuibia. Zito kumtuhumu muheshimiwa raisi na serikali yake kuwa inawaibia watanzania kwa kweli ni upuuzi uliokithiri.

    ReplyDelete
  2. Hilo neno unafikiri watanzania ni m*********a si zuri tafsiri yake ni mambo yahusuyo imani za kichawi na ushirikina. Kamwe lisiendekezwe kwenye ngazi yoyote ya jamii ya Tanzania.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad