Aisee Bongo Movie Bado Sana Tusubiri miaka 1000..Ona Huyu Mdada Anayelipwa Bilioni 5 Kwa Kila Episode ya Series

Kwa wale watazamaji wa series ya game of thrones kuna mwanadada anajulikana kama Daenarys Targaryen ambaye jina lake halisi ni Emilia Isabelle Euphemia Rose Clarke, raia wa Uingereza kazaliwa mwaka 1986.

Huyu dada analipwa Euro milion 2 kwa kila epsode anayoshiriki ambazo kwa pesa yetu ya madafu ni sawa na bilion 5.45. KIla series ya game of thrones inakuwa na epsodes nane ina maana akionekana kwenye epsodes zote kitu ambacho mara nyingi uwa inakuwa hivyo anakuwa kavuta bilion kama 50 za kibongo.

Mpaka Mbongo movie ije kufika hapa ni miaka 1000 ijayo.
Malipo hayo ni kwa mtu mmoja sasa jiulize GOT ilivyo na characters wengi sijui budget yake itakuwa kiasi gani.

Lakini ela itakuwa inarudi maana ndiyo series ambayo kila season ikitoka inavunja rekodi ambayo uwa inaiweka yenyewe yani GOT ndiyo series inayofuatiliwa zaidi na imekuwa kuwa ikivunja rekodi yake yenyewe kwa kuongoza watazamaji kila season yani toka ianze kutoka kila season watazamaji wanaongezeka badala ya kupungua na pia ndiyo series inayovunja rekodi kwa kudownloadiwa kiwizi wizi.

SOMA Pia: Job Opportunities at Fastjet Tanzania, Cabin Crew

Top Post Ad

Below Post Ad