Alishtaki Kanisa kwa Kumtaka Akabidhi Majibu ya UKIMWI kabla ya ndoa

Michael Aboneka raia wa Uganda amefungua kesi katika mahakama ya katiba mjini Kampala dhidi ya kanisa la Watoto Church akilalamikia utaratibu mgumu wa kufunga ndoa anaodai unaenda kinyume na katiba ya nchi hiyo huku waumini wengine wakiunga mkono utaratibu huo.

Taratibu anazozipinga za kanisa hilo za kufunga ndoa ni pamoja na kuwa ni lazima jamaa huyo apate barua ya kuridhia ndoa hiyo kutoka kwa wazazi wa bibi harusi ambayo wanaita Baraka kitu anachodai ni kinyume na kifungu 31 ya katiba ya nchi.

Lakini pia utaratibu mwingine unaomkwaza kijana huyo ni kutakiwa kuwasilisha majibu ya vipimo vya UKIMWI ya yeye na mpenzi wake kanisani ambapo amesema ‘inavunja uhuru wa faragha wa yeye na mpenzi wake.

Aidha kanuni nyingine mwiba kwa Michael ni ile ya kutakiwa kusubiri miezi sita baada ya kuomba kufanya harusi na kulipa ada ya kanisa shilingi laki nne na nusu za Uganda sawa na laki tatu na elfu ishirini na tano za kitanzania.

Licha ya Michael kupinga utaratibu huo anaodai unawanyima haki ya vijana wengi kufunga ndoa waumini wengine wanaona ni sawa tu utaratibu huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad