Aliyewatumbua Wenye Elimu ya Darasa la saba Naye Atumbuliwa

Aliyewatumbua Wenye Elimu ya Darasa la saba Naye Atumbuliwa
Mkurugenzi mtendaji  wa halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga Peter Nyalali  amemsimamisha kazi kaimu afisa utumishi wa halmashauri hiyo Protas Dibogo kwa kosa la kukaidi kuwarudisha kazini watendaji wa vijiji 41 baada ya serikali kuagiza warejeshwe.


Nyalali ametoa kauli hiyo wakati wa kikao chake na watumishi wa halmashauri hiyo ambapo, pamoja na mambo mengine amesisitiza watendaji hao kwenda kufanya kazi kwa bidii kwenye maeneo yao mara tu watakaporejea kazini.

Hivi karibuni serikali iliagiza kurudishwa kazini kwa watumishi wote walioajiriwa 01/05/2004, ambapo  Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Bumbuli Peter Nyalali  alimwagiza kaimu afisa utumishi wa halmashauri hiyo awarudishe kazini watendaji wa vijiji 41.

Pamoja na kutolewa agizo hilo Kaimu Afisa Utumishi Protas Dibogo hakutekeleza agizo hilo jambo lililosababisha  Mkurugenzi Nyalali kumsimamisha kazi.

"Masharti yanaonyesha kwamba nyie mmeanza tarehe 1 mwezi 5. Yeye anapotosha hapa anasema kwamba mmeanza mwezi wa 6. Ninamsimamisha kazi na nafasi yake atakaa Bi Asha Majid" Nyalali.

Tarehe 01/05/2004 serikali iliwaajiri watumishi waliokuwa wakijitolea katika maeneo mbalimbali nchini,ambapo  tarehe 20/05/2004 serikali ilitoa kibali cha kuajiri watumishi wapya wenye elimu ya darasa la saba huku ikiwataka kujiendeleza wawapo kazini
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad