Askari walikuwa wamejikusanya mbele ya kituo chao cha Polisi wamejiunga na waandamanaji Paris wanaoandamana kwa muda wa siku kadhaa wakipinga siasa za rais Emmanuel Macron.
Askari hao wamedai kuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu huku wakikabiliwa na tatizo la mishahara. Vile vile wametoa malalamiko kufanya kazi muda mrefu bila ya kupata muda wa kutosha wa kuwa na familia zao.
Katika maandamano hayo, askari polisi wameomba kuajiriwa kwa askari wapya.
Maandamano hayo nchini Ufaransa kwa sasa yanakaribia kutimiza miezi mitatu tangu kuanza kwake.