Baby J Afunguka Ukweli Mchungu "Kiukweli kuolewa na staa ni stress"

MSANII wa Bongo Fleva kutoka Zanzibar, Jamila Abdallah ‘Baby J’, aliyewahi kutamba na ngoma za Bwashee Bwashee, Mpenzi Wangu pamoja na Moyo Wangu amesema kwamba kuolewa na mtu maarufu ni ‘stress’ kwani wengi huwa hawajatulia.

Baby J, ambaye anatarajia kuibuka na ujio mpya na mwanamuziki MwanaFA, aliongeza kuwa kwa upande wake ni vigumu kuolewa na staa kwa sababu amewahi kuwa kwenye uhusiano na staa ambaye hakupenda kumtaja jina na ameona ugumu wake.

“Kiukweli suala la kuolewa na staa kwa upande wangu ninaona kwamba ni stress tu, mastaa wengi hawajatulia. Nimekuwa kwenye uhusiano, ninafahamu kwa hiyo sidhani kama itatokea kuolewa na mtu maarufu!”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad