Bilali Mashauzi Kuzikwa Leo Upanga, Dar

Bilali Mashauzi Kuzikwa Leo Upanga, Dar
MWIMBAJI wa muziki wa taarab wa kundi la  Mashauzi Classic, Bilal Mashauzi, amefariki  jana na atazikwa leo Upanga jijini Dar es Salaam.

Familia yao imeishi kwa miaka mingi, Upanga mtaa wa Wibu  hadi  na baadaye waliposhindwana na mwenye nyumba miezi ya karibuni na wakahamia Mwananyamala ambapo yeye ndiye alikuwa kichwa cha familia.

Bilal Mashauzi enzi za uhai wake alikumbwa na kashfa ya kujihusisha na vitendo vya ushoga.

Wakati Isha Mashauzi anaanzisha Mashauzi Classic alimuomba Bilal hilo jina la Mashauzi na marehemu akaridhia ndipo kundi hilo lilipotambulishwa kwa jina la Mashauzi Classic.

Bilal amezaliwa na kukulia mitaa ya Togo, Kinondoni na Wibu, Upanga.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad