Msanii wa filamu bongo, Daudi Michael maarufu kama 'Duma' amefunguka na kudai kuna wasanii wengi katika 'industry' muvi hawana akili timamu ila wanawavumilia kwa kuwa ndio uwezo wao umeishia hapo.
Duma ametoa kauli hiyo wakati akizungumza mbele ya kamera za eNewz kutoka EATV baada ya msanii Gabo Zigamba kutoa kauli yake iliyozua utata mzito kuwa anahitajika atengenezwe Kanumba mwingine ndani ya filamu za bongo ili aitendee haki tasnia hiyo licha ya Gabo kudai hakuwa na maneno yake hayakuwa na maana kama walivyoyapokea baadhi ya wasanii na mashabiki wa filamu nchini.
"Kama kweli unajiamini wewe ni msanii mzuri, unawezo, unajituma na kupambana huwezi kusema unahitaji Kanumba mwingine. Kwani sisi hatuwezi alichokifanya Kanumba, unajua sio kila star ana akili timamu wengine ni mitambo tupo nao katika industry' lakini uwezo wao ndio umeishia hapo", amesema Duma.
Pamoja na hayo, Duma ameendelea kwa kusema "kama unajiamini, kujituma na unaweza kufanya kazi kubwa zaidi kwasababu hata hawa viongozi wetu wa nje wanabadilisha kila siku Mawaziri wanakuja wakubwa na wafanya kazi zaidi ya wale waliotangulia kwanini useme hivi hivyo na sisi tuishie hapo hapo".