MTWARA: Mahakama Kuu leo imetoa zuio la muda(Temporary Injuction) dhidi ya matumizi ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao (Online Content Regulations)
Kanuni hizo matumizi yake yamekwishaanza na tarehe ya mwisho ya bloga na mitandao kuridhia ilikuwa kesho Mei 5, 2018
Maombi hayo yaliyowalishwa mahakamani na waombaji 6 wakiwemo Jamii Media, Legal and Human Rights Cente(LHRC), THRDC, MCT, TAMWA na TEF
Katika kesi ya msingi ya mapatio ya kanuni hizo(Judicial review) washitakiwa ni Waziri wa Habari, Tanzania Communication Authority (TCRA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG)
Katika maombi ya msingi waombaji wameiomba Mahakama kufanya mapitio ya kanuni hizo kwa vigezo hivi:
i) Waziri ametumia nguvu ya kisheria nje ya mamlaka yake (Ultra vires)
ii) Zinakiuka kanuni za usawa (Natural justice)
iii) Kanuni hizo zinapingana na Uhuru wa kujieleza (Freedom of Exepression) Haki ya kusikilizwa(Rights to be heard) na haki ya usiri( Right to Privacy)
Kesi ya msingi imepangwa kusikilizwa Mei 10, 2018