Bulembo Ahoji Kigugumizi Cha Mwijage Kwa Wamiliki Wa Viwanda

Mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo (CCM), amemtaka Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuweka kando kigugumizi alichonacho katika kuwanyang’anya wamiliki wa viwanda walioshindwa kuviendeleza.

Bulembo ametoa kauli hiyo jana  Mei 11, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2018/19, na kuongeza kuwa inashangaza kuona Mwijage anashindwa kuwachukulia hatua wamiliki hao ilihali tayari Rais John Magufuli alimwagiza kutekeleza agizo hilo mara kadhaa.

“Viwanda vingi vilibinafsishwa na wamiliki wengi wameshindwa kuviendesha, serikali na Rais magufuli amekuambia wanyang’anye… kuna watu wamepewa vina mashine lakini hakuna kitu.

“Baadhi ya viwanda kule Dar es Salaam, Mara , Lindi na Bukoba, wamiliki wamevichukua na kuvigeuza kuwa maghala, sasa unaogopa nini kuwanyang’anya ilihali tayari wamekiuka masharti ya mkataba,” alisema Bulembo.

Bulembo alisema watendaji walioko chini ya waziri wanamhujumu Mwijage kwa kuwa wanaamini nafasi ya uwaziri ni ya kisiasa kwa kuwa baada ya miaka mitano atakuja kiongozi mwingine.

“Ukipanga nyumba ya mtu ukakuta ina nondo kesho ukiweka mbao mwenye nyumba akikufukuza utampeleka mahakamani? wengine wana viwanda wanachechemea afadhali hao kuliko ambao wamebadilisha matumizi,” amesema.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad