Bwawa la Kutengeneza Lapasuka na Kuuwa Watu 27 Kenya


NAKURU, KENYA: Watu 27 wamefariki huku wengi wakiwa hawajulikani walipo na wengine zaidi ya 2000 wakiachwa bila makazi baada ya bwawa la Patel kuvunja kuta zake jana Mei 09, usiku

Waliokiwa jirani na eneo la bwawa hilo wanasema walisikia mshindo mkubwa kabla ya maji mengi kuanza kusomba makazi na mashamba ya watu umbali wa kilometa mbili kutoka bwawani

Kuna hofu kwamba huenda idadi ya watu waliofariki ikaongezeka wakati jitihada za uokoaji zikiendelea

Bwawa hilo la Patel ni mojawapo ya mabwawa matatu yanayomilikiwa na mkulima mmoja mkubwa katika eneo hilo

Chanzo cha kuta za bwawa hilo kupasuka inaarifiwa kuwa ni maji mengi kujaa baada ya kukusanyika kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad