Mkuu wa zamani wa uchunguzi wa chanzo cha vifo nchini Kenya ameshtakiwa kosa la kuiba moyo kutoka kwenye maiti iliyokuwa inafanyiwa upasuaji.
Dkt. Moses Njue alikanusha shitaka hilo aliposomewa mashitaka yake katika Mahakama ya Hakimu Mkuu Nairobi ambapo alikuwa ameshitakiwa yeye na mwanae pamoja msaidizi wake.
Walidaiwa kuiba moyo wa Timothy Mwandi Muumbo wakifanyia mwili wake upasuaji Juni 25, 2015 katika chumba cha kuhifadhia maiti cha 'Lee Funeral Home'.
Hakimu Mkuu Francis Andayi aliagiza watuhumiwa wengine wafike Mahakamani na kujibu mashitaka kabla ya kesi kuanza kusikilizwa Julai 3.
Dkt. Njue alikanusha pia shitaka jingine la kuuharibu moyo ili kuficha ushahidi, akifahamu kwamba ripoti ya uchunguzi wa maiti hiyo ingetumiwa kwenye kesi iliyokuwepo Mahakamani.