Davido Awajibu Mashabiki Wanaosema Kapenda Ghafla

Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido leo akisherehekea Birthday ya mpenzi wake ameamua kuweka wazi kuhusiana na mahusiano yake ya kimapenzi na Chioma ambaye amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Davido ambaye amewashtua mashabiki wengi na kuanza kuhoji kuwa kapenda ghafla, baada ya kuamua kumpost mpenzi wake Chioma na kumzawadia gari jipya aina ya Porshe yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 200 wakidhani kuwa ni mapema sana kufanya hivyo

Davido kupitia twitter account yake amewajibu walihoji kuwa kapenda ghafla kwa kusema kuwa “kama kuwa na mtu katika mahusiano kwa miaka mitano ni kupenda ghafla basi sawa” Kwa sasa Davido ana watoto wawili ambao amezaa na wanawake wawili tofauti ambaye mmoja alizaa na Momodu na mwingine alizaa na Amanda.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad