Dunia Kusimama kwa Dakika 90 Kuiona Real Madrid vs Liverpool hii leo

Real Madrid vs Liverpool hatimaye siku imefika, hii ni fainali ya 16 kwa Real Madrid maarufu kama Los Blancos katika michuano ya barani Ulaya, na hakuna klabu ambayo imewafikia wababe hawa wa Madrid katika rekodi hii.

Wakati Real Madrid wakiwa na rekodi hiyo, wapinzani wao siku ya leo Liverpool wenyewe wamekwenda fainali za barani Ulaya mara 7 na ni ya 8 na ndio klabu ya nchini Uingereza ambayo imekwenda fainali za Ulaya mara nyingi zaidi.

Ukiacha mwaka 1962 ambapo Real Madrid walifungwa na Benfica katika fainali hizi, 1964 walipofungwa na Inter Milan na 1981 walipofungwa na Liverpool, fainali zingine zote 12 zilizobaki Real Madrid waliibuka kidedea.

Wakati Real Madrid wenyewe wamepoteza katika fainali 3 kati ya fainali 15 ambazo wameshacheza, majogoo wa London Liverpool wenyewe wamepoteza fainali 2/7, Liverpool walipigwa na Juventus 1985 na wakafungwa na Ac Milan mwaka 2007.

Hii ya leo ni fainali ya tatu mfululizo kwa Real Madrid kucheza katika Champions League, lakini Real Madrid sio wa kwanza kufanya hivi kwani mwaka 1996-1998 klabu ya Juventus ya nchini Italia nao walifika fainali mara 3 mfululizo za Champions League.

Tangu Liverpool wawafunge Real Madrid katika fainali za UEFA mwaka 1981 Los Blancos hawajawahi kupoteza katika fainali sita zilizofuatia za michuano ya Champions League walishinda 1998, 2000, 2002, 2014, 2016 na 2017.

Tangu baada ya Liverpool kuifunga mabao 5-4 Alaves katika michuano ya UEFA Cup mwaka 2001, timu za kutoka nchini Hispania hazijawahi kupoteza fainali hata moja ya michuano mikubwa Ulaya dhidi ya timu za kutoka Uingereza.

Wakati karibia kikosi chote cha Real Madrid hii leo wamewahi kushiriki fainali ya Champions League, hali ni tofauti kwa Liverpool kwani kikosi chao kizima hii leo hakuna mchezaji aliyewahi kucheza fainali hizi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad