Fahamu Jinsi ya Kujiokoa Katika Dharura ya Moto Nyumbani Mwako

Ajali  ya moto imekuwa ikitokea mara kwa mara, muda mwingine matatizo haya huja bila taarifa, inapotokea dharura ya moto ndani ya nyumba unatakiwa kujua mambo yafutayo:

Kitu cha muhimu ni kutoka nje salama haraka iwezekanavyo (as soon as possible).
Hakikisha  kila siku mlango wa dharura wa nyumba  umekaa kwa urahisi sehemu ambayo imekaa mahali ambapo ni karibu, na pia uwe ni malngo ambao unagumgukia nje. Lakini pia Kila mtu ajue funguo za milango ya kutokea zinapowekwa, sio zinafichwa.

Fahamu kwamba ktk matukio mengi ya moto kinachoua ni moshi kabla ya moto, hivyo ukiona dalili ya moshi hakikisha unakuwa na kitambaa kibichi cha kujifunika puani na mdomoni, na kama moshi umeanza kuingia ulipo tambaa chini (crawl down) sababu hewa ya uhai (oxygen) ina uzito (density) kubwa kuliko hewa ya kifo (carbon monoxide) hivyo inakuwa imekandamizwa chini sentimita chache kutoka kwenye sakafu (few centimeters from the floor). Hivyo tembea kwa kutambaa.
Hakikisha unawajulisha watu wote ambao wamelala ili kama wamelala ili waweze kutoka nje haraka.
Achana na fikra ya kuokoa vitu, katika hatua hii cha muhimu ni kuokoa uhai kwanza.
Kumbuka, muda ni kitu cha msingi, fanya haraka iwezekanavyo (quick as possible) katika kujiokoa na kuokoa wengine.

Ni muhimu nyumba zetu kuziwekea kiashiria moshi (smoke detectors) na pia kizima moto (fire extinguishers). Kugundua haraka (early detection) ya moto ni muhimu sana ili kuweza kuudhibiti kirahisi. Smoke detector ni mashine ya elektroniki ambayo inagundua moshi ktk hatua ya mwanzo kabisa na itapiga kelele (alarm) kwa sauti ya juu, itakusaidia kuamka hata kama upo usingizini na kuweza kujiokoa na kuokoa wengine na kuuzima moto kabla hujashika kasi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad