Familia Yatangaza Ratiba ya Mazishi ya Mdogo wa John Heche

Familia Yatangaza Ratiba ya Mazishi ya Mdogo wa John Heche
Serikali mkoani Mara pamoja na familia ya Chacha Suguta aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi juzi, wanatarajia kukutana na waandishi wa habari leo mchana kwa ajili ya kutangaza taratibu na ratiba ya mazishi ya  kijana huyo.

Kikao cha familia pamoja na uongozi wa Serikali kinafanyika baada ya pande hizo mbili kukutana jana na kufikia makubaliano yatakayotangazwa rasmi kwa umma baadaye mchana.

Mbunge wa Tarime, John Heche amesema familia hiyo pia inatarajia kutangaza msimamo wake kuhusu hatua za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya askari William Marwa (50) anayedaiwa kumuua Chacha.

Soma: Familia ya Heche yasubiri kikao na polisi kumzika ndugu aliyeuawa

Askari huyo hata hivyo alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Tarime jana na kusomewa shtaka la mauaji.

Tukio hilo lilitokea Aprili 27 mwaka huu baada ya Suguta kukamatwa na polisi usiku akiwa katika baa ya Kasablanca na kupelekwa mahabusu.

Hata hivyo asubuhi ndugu zake walipokwenda kumuangalia, waliambiwa ameshafariki na mwili upo mochwari.  Kesi hiyo itatajwa tena Mei 15 mwaka huu.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad