“Ningekuwa shabiki wa Yanga sidhani kama ningeefurahi kusikia Simba imemsajili Adam Salamba na Marcel Kaheza, Azam wamemsajili Ngoma, halafu Yanga ambayo inatakupambania ubingwa msimu ujao inamsajili Ngasa.”
“Wakati wa pinzani wa Yanga (Simba na Azam) wanasajili wachezaji wanaoweza kuwatumia kwa muda mrefu (Kaheza, Salamba, Kutinyu, Mudathir) Yanga wao wanarudi nyuma kwa Ngasa lakini nasikia kuna story kwamba huenda Salum Telela akarudishwa hizi sio ishara nzuri kwa Yanga.”
“Ngasa sio mchezaji mbaya lakini Ngasa yule aliyetoka Yanga akaenda Azam, Simba, akaenda nje si huyu wa sasa, anahitaji kuni-prove wrong”.
Ngasa atacheza Yanga kwa mara ya tatu katika vipindi tofauti, mara ya kwanza alisajiliwa akitokea Kagera Sugar, akafanya vizuri akaenda Azam baadaye wakamtoa kwa mkopo kwenda Simba muda wake ulipomalika akarudi Yanga.
Baada ya kurudi Yanga mara ya pili alirudi kwenye ubora wake hatimaye akapata fursa ya kucheza Free State Stars ya South Afrika ambako alivunja mkataba na kwenda Fanja ya Oman na kurudi Bongo akasajiliwa na Mbeya City na baadaye Ndanda kabla ya kurudi tena Yanga.