Meneja wa Wales Ryan Giggs anasema anatumai na anaomba meneja wake wa zamani Sir Alex Ferguson ataweza kupona uvujaji wa damu ubongoni.
Ferguson, mwenye umri wa miaka 76, bado yupo katika hali mahututi baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura siku ya Jumamosi.
Meneja huyo wa zamani alimruhusu Giggs wakati huo akiwana miaka 17 kucheza kwa mara ya kwanza katika timu ya Manchester United mnamo 1991 na alikuwa katika kikosi cha kwanza cha mechi 13 za Ferguson na kushinda mataji ya Premier League.
"Sasa ni wakati wa kumuombea na kutamaini kuwa atapona kikamilifu," Giggs ameiambia BBC Wales.
"Amekuwa na ushawishi mkubwa katika kazi yangu ndani na hata nje ya uwanja.
"Najua upasuaji ulikuwana ufanisi - lakini yeye ni mpanaji na hilo ndilo linalonifanya nikafikiria kuwa ataweza kupona."
Meneja wa sasa wa Manchester United na mlinzi wa timu ya taifa ya England Phil Jones, pia ametuma ujumbe kama wa Giggs kwamba anamuombea Ferguson na amemtaja kama babake.
Jones alisajiliwa kutoka Blackburn na Ferguson akiwa na umri wa miaka 19 mnamo Juni 2011 na alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda cha mechi yake ya mwisho kabla astaafu mnamo Mei 2013 baada ya kushinda mataji 38 katika muda aliyohudumu wa miaka 28 katika klabu hiyo.
"Alinishukulia kama mtoto wake, na lilikuwa jambo la kushangaza," amesema Jones, mwenye umri wa miaka 26.
"Inahuzunisha lakini namjua, na atapambana vilivyo."
Michael Carrick, aliyecheza chini ya ukufunzi wa Ferguson kwa miaka 7 na anapokea ukufunzi wa wa klabu hiyo amesema amuhuzunishwa sana kusikia taarifa kuhusu Ferguson.
Mameneja katika ligi ya England akiwemo wa Arsenal, Arsene Wenger na wa Manchester City's Pep Guardiola, wote walituma ujumbe na maombi mwishoni mwa juma kwa Ferguson, ambaye anasifika kuwa Meneja mwenye ufanisi mkubwa katika historia ya soka Uingereza.
Wenger, ambaye anaondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu, amemtaja Ferguson kama 'mtu mwenye matumaini ' huku Guardiola akisema anamfikira sana mkewe Ferguson Cathy na familia yake nzima akiwemo mtoto wao Darren, ambaye kwa sasa anaisimamia timu ya Doncaster Rovers.