Haji Manara Afunguka Haya Kuhusu Alikiba, Diamond

Haji Manara Afunguka Haya Kuhusu Alikiba, Diamond
Msemaji wa Simba SC, Haji Manara amewataka wasanii kuwa na nidhamu na kuacha kulewa umaarufu mdogo walioupata kwa muda mchache.

Manara ameyasena hayo Jumamosi hii wakati akiwa Wilayani Pangani kwaajili ya uzinduzi wa kombe la Aweso Cup litakalozinduliwa kwa mechi ya mashabiki wa Simba na Yanga.

“Nidhamu itaijengea heshima tasnia yenu, kuna baadhi ya watu wanaharibu tasnia yenu, unajua ukishapata ustaa kidogo unajiona kama Mungu mtu, lakini ustaa unapita tu,” amesema.

“King Kiki alikuwa akiingia sharti ukumbi mzima unasimama, juzi nilikuwa nawaambia kina Alikiba na Diamond nyie hamjafikia ustaa wa King Kiki, yuko wapi?, ustaa unakuja na kuondoka,” amesisitiza Haji.

Top Post Ad

Below Post Ad