Hatimaye Nchi ya Saudi Arabia yaruhusu Ujenzi wa Makanisa Baada ya Katazo la Muda Mrefu


Nchi ya Saudi Arabia imeamua kuruhusu ujenzi wa makanisa baada ya kusainiwa kwa makubaliano kati ya viongozi wa Wahhabi na Kadinali wa Vatican.

Makubaliano hayo kati ya Rais wa Baraza la Kipontifiki ya midahalo ya dini mbalimbali, Kadinali Jean-Louis Tauran na Sheikh Mohammed bin Abdel Karim Al-Issa, ambaye ni Katibu Mkuu wa NGO kubwa ya Wahhabi yanalenga kuruhusu ujenzi wa makanisa pamoja na mikutano ya Waislamu na Wakristo mara moja kila baada ya miaka miwili.

Saudi Arabia ni moja ya nchi zisizo na uvumilivu kwa dini nyingine zaidi ya Uislamu. Wasio waislamu wanaadhibiwa kwa kuonesha matendo ya dini yao nje ya nyumba zao huku Muislamu yeyote anayeamua kubadili dini akihukumiwa kifo. Sheria za kiislamu zinawahusu wote wanaoishi nchini humo bila kuzingatia imani zao huku Jeshi la Polisi likisimamia ufuatwaji wake.

Hadi sasa inakadiriwa kuwa kuna Wakristo zaidi ya Milioni 1.5 nchini humo ambao ni wahamiaji wanaofanya kazi hususani kutoka nchi ya Ufilipino.

Uwezekano wa ufanikiwa kwa harakati hizi za Vatican zilizoanza mwaka 2008 ulianza kuonekana baada ya Mwanamfalme Mohammed bin Salman kuingia madarakani ambapo amedhamiria kubadili muonekano wa nchi hiyo kimataifa kwa kubadili mambo kadhaa.

Katika kipindi chake tayari ameshabadili taratibu kadhaa zilizokuwepo kwa miaka mingi kama wanawake kutoruhusiwa kuendesha magari na kutakiwa kuwa na mwangalizi muda wote.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad