Hivi Hawa Wasanii wa Kike Kwanini Hawawezagi Kujitungia Nyimbo?

Nimefatilia sana hawa wasanii wa kike waliopata kuwa na majina makubwa tangu zamani kama Ray C, Mwasiti, Linah, Rachel, Vumilia, Qeen Darlin, Pipi, Shilole, Snura, Vanessa Mdee, Ruby, Maua Sama, Nandy, Giggy, Mimi Mars, Amberlulu, n.k kwenye mahojiano kwa nyakati yofauti wakisema kutungiwa nyimbo zao na watu kama Barnaba, Amini, Ditto, Mario, etc tena sio kutungiwa tu wakati mwingine wanapewa hadi melody 'wanapita mulemule', je pengine hii ndio sababu huwa hawadumu sokoni?

Tatizo nini hasa, mfano juzi nimemsikia Nandy anasema huo wimbo wake mpya alikuwa ameufanya Aslay akapewa, kwangu mimi huyu sio mwanamuziki bali ni mwimbaji. Kuandikiwa nyimbo sio tatizo, hata kule mbele wasanii wakubwa sometimes wanaandikiwa, but kutegemea 100% kuandikiwa wakati mwingine kupewa na melody kuna shida hapa.

Nadhani udhaifu wa wasanii wengi wa kike ndio kunafanya kukosekane wa kukaribia legacy ya Lady Jaydee, wengi ni wasanii wa kutengenezwa na sio vipaji, na hii ndio ilichangia hata Rubby kuyumba sana alipotoka kwa kina Ruge, alizoea kupikiwa kilakitu yeye anaingiza vocal tu.

By Screpa

Top Post Ad

Below Post Ad