IGP Awaagiza Wananchi Kuwakamata na Kuwakapiga Mawe Askari Wasiojitambulisha

IGP Awaagiza Wananchi Kuwakamata na  Kuwakapiga Mawe Askari Wasiojitambulisha
MKUU jeshi la polisi nchini Uganda amewaamrisha wananchi kuwakamata au kuwapiga mawe maofisa wa polisi wasiojitambulisha wanapokwenda kuwakamata washukiwa hata kama wamebeba bunduki.



Raia wa Uganda wamedai kwamba wanashindwa kuwatambua wanaowateka jamaa zao kwani wana tabia sawa na za maofisa wa polisi, wanaowakamata raia bila ya kujitambulisha, wala kuvaa sare za kikazi.



“Polisi anastahili kujitambulisha na kumweleza mshukiwa sababu za kumkamta kabla ya kumkata. Kama hafanyi hivyo, raia wawakamate au wawapige mawe,” amesema Kamanda Okoth Ochola.



Karibu kila siku, matukio ya mtu kutekwa, hasa wasichana na akina mama yamekuwa yakiripotiwa nchini Uganda. Utekaji pia umesambaa na kuwalenga watoto wadogo, chini ya miaka mitano licha ya maofisa wa polisi na jeshi kuingilia kati kukabiliana na watekaji. Mkuu wa polisi anahusisha utekaji nyara huo na makundi ya kigaidi.



“Baadhi ya washukiwa ambao tumewakamata wana uhusiano na makundi ya kigaidi lakini sitayataja kwa wakati huu kwa sababu bado tunafanya uchunguzi. Tutakapokamilisha uchunguzi wetu, tutawaeleza,” alisema Ochola.



Visa vya utekaji watu vimekuwa vikiendelea nchini Uganda kwa mda wa takriban mwaka mmoja sasa. Watekaji hudai mamilioni ya pesa kama ili kuwaachia mateka, na hata baada ya kulipwa pesa wanazotaka, huwaua watu waliowateka.



Wakati huohuo, polisi nchini Uganda wamewakamata wapiganaji wa Maimai 26 kutoka Jamhuri ya Kidemokraksia ya Congo (DRC), baada kikundi cha wapiganaji hao kuwateka wavuvi sita raia wa Uganda katika Ziwa Edwward, magharibi mwa Uganda. Wapiganaji wa Mai Mai wanataka kupatiwa masanduku kadhaa ya risasi ili kuwachia mateka.



“Pamoja na hayo na sisi, tumewakamata wapiganaji wao 26. Kwa hivyo tumewapa masharti kwamba waachilie raia wetu kwanza,” amesema Ochola.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad