Inasikitisha Wanakijiji 10 Wameuawa kwa Kukatwa Vichwa

Inasikitisha Wanakijiji 10 Wameuawa kwa Kukatwa Vichwa
Wanavijiji wapatao 10 wameuawa kwa kukatwa vichwa mwishoni mwa wiki iliyopita na watu wanaosadikiwa kuwa ni Waislamu wenye msimamo mkali wa kidini katika Jimbo la Kaskazini mwa nchi.
Watoto ni miongoni mwa watu ambao wanalengwa katika shambulio lililofanyika kijiji cha Monjane, mkoa wa Cabo Delgado, aneo ambalo ni maarufu kwa shughuli za uchimbaji madini na utafiti wa mafuta.
Kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu kiliripotiwa kufanya mashambulizi ya kushtukiza katika eneo hilo mwaka jana. Inaaminika kikundi hicho kinajipatia mamilioni ya dola kwa kuuza mbao na madini ya rubi.
Kikundi hicho, ambacho wenyeji wanakiita al-Shabab, kilianzishwa mwaka 2015 kama shirika la kidini na hakuna taarifa rasmi ikiwa kina uhusiano na kikundi cha wapiganaji wa jihadi wa Somalia wanaotumia pia jina hilo.
Mmoja wa waathirika wa shambulizi hilo lililofanywa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye kijiji cha Monjane aliliambia shirika la habari la AFP: "Walimlenga mkuu wa kijiji kwa kuwa amekuwa wakiwapatia taarifa polisi kuhusu mahali ambako al-Shabab wamejificha msituni.”
Utafiti wa kisomi wa hivi karibuni, ukiwemo uliochapishwa wiki hii katika majarida ya habari na makala fupifupi, ulibaini kwamba wafuasi wa mwanzo wa kikundi hicho ambao wakati fulani wanaitwa al-Sunna, walikuwa wafuasi wenye msimamo mkali wa mhubiri wa Kenya aliyeuawa mwaka 2012.
Wafuasi wake walihamia Kusini na wakaenda kuweka makao Kibiti Kusini mwa Tanzania na karibu na mpaka na Msumbiji.
Polisi wamefanikiwa kuwakamatwa zaidi ya watu 200 wakihusishwa na mashambulizi ya wapiganaji wa Kiislamu kuanzia Oktoba mwaka jana.
Wiki iliyopita, mamlaka zilifungua misikiti sita ambayo ilikuwa imefungwa katika kipindi yalipohanikiza mashambulizi baada ya kukataa mafungamano na wapiganaji hao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad