Jaji Amuonya Rais Trump Kuhusu Mitandao ya Kijamii

Jaji Amuonya Rais Trump Kuhusu Mitandao ya Kijamii
Hakuna ubishi kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump ni moja ya Marais maarufu zaidi kwenye mitandao ya kijamii kwani haipiti siku bila Rais huyo kuposti au kutweet.

Sasa habari mbaya kwake ni kwamba Jaji wa Jiji la New York, Naomi Reice Buchwald amesema kuwa Rais huyo anatakiwa kuwa mvumilivu na mnyenyekevu kwenye mitandao ya kijamii hasa pale anapokutana na watu wanaompinga, kumkejeli na kumtolea lugha za matusi kwani yeye ni kiongozi wa taifa na anawajibu wa kumsikiliza kila mtu.

Buchwald kwenye taarifa yake aliyoitoa juzi Mei 23, 2018 amesema Rais Trump hatakiwa kabisa kum-block mtu yeyote kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, kwani kufanya hivyo ni kuvunja katiba ya nchi. Soma taarifa ya Jaji Buchwald hapa chini.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad