Mimi nipo kwenye tasnia ya elimu hasa shule binafsi za International..
Nimeshuhudia watoto wanaanzishwa shule wakiwa na umri wa miaka 3 hadi 4 na anafuatilia kitaaluma hivyo harudii darasa. Matokeo yake anamaliza shule bado mdogo sana.
Kuna watanzania bado wanasubiri mtoto afike miaka 7 ndio aanze shule?
Kama ni kwa sababu za kiuchumi, siku hizi kuna Nursery Schools hata mitaani. Nashauri umpeleke mwanao na umfatilie ili asiizoee shule, awe serious nayo. Kwa kufanya hivyo, atamaliza elimu akiwa mdogo na itamsaidia kwenye soko la ajira.
Pia tenga muda wa kumpa tuition, hata kama yupo darasa la 2. Kaa nae hata 1 hour kwa siku, mfundishe vitu vya darasa la 2 na au la 3.
Asanteni
By Gentleman P/JF