Jerry Muro Atuma Maombi Yanga "Tumeni Mapumziko CAF Ili Mpumzike Mashindano ya Kimataifa"

Jerry Muro Atuma Maombi Yanga "Tumeni Mapumziko CAF Ili Mpumzike Mashindano ya Kimataifa"
Mkuu wa zamani wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika klabu ya Yanga, Jerry Muro, amewaomba Yanga kutuma maombi Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) ili wapumzike kushiriki mashindano ya kimataifa.

Muro ambaye aliwahi kukalia kiti hicho kabla ya kuja kuchukuliwa na Dismas Ten ambaye ndiye Afisa Habari wa sasa, amesema ili Yanga waweze kufanya vizuri, njia pekee ya kufanya ni kupumzika kushiriki mashindano hayo.

Kiongozi huyo wa zamani wa Yanga, ameeleza kuwa Yanga hivi sasa wanakuwa kama wanacheza mechi za kirafiki tu huku hakuna dalili zozote zinazoonesha kama itafanya vizuri.

Muro anaamini kama Yanga watapumzika na kusajii wachezaji wenye hadhi ya kimataifa kama uhalisia wa jina kubwa na timu lilivyo, itaweza kuonesha ustahimilivu wa kutosha kuliko kusajili wachezaji ambao hawana hadhi ya kuchezea Yanga.

Ushauri wa Muro kwa Yanga amewataka wafanye hivyo ili waweze kujipanga upya angalau baada ya miaka mitatu mpaka minne kisha warejee katika michuano hiyo ya kimataifa.

Kauli hiyo ya Muro imekuja kufuatia kikosi cha Yanga kukubali kufungwa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya U.S.M Alger katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika huko Algiers, Algeria Jumapili ya Mei 6 2018.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad