JPM Sio Mtu wa Mchezo.. Afunguka"Huyo Nitalala Naye Mbele Mwenyewe"

Rais Magufuli amewataka Wakulima na Wafugaji kuacha vitendo vya kupigana na kwamba katika serikali yake hakuna mtu aliyeko juu zaidi ya mwingine na kusisitiza kwamba watanzania wote ni sawa kwani ndiyo waliyomchagua.


Akizungumza na wananchi wa Morogoro akiwa njiani kuelekea Msamvu Raid Magufuli amesema kwamba kamwe vitendo vya kupigana visirudie katika serikali yake na kwamba wale watakaokiuka watashughulikiwa.

Aidha ameongeza kuwa anataka wakulima na wafugaji waishi kwa kuheshimiana kwani yeye anachokihitaji ni amani.

Pamoja na hayo, Rais Magufuli amewashangaa Wafugani kuwalisha ng'ombe mazao ya wakulima ilhali kuna majani ya kutosha na wanaposhtakiwa wanaamua kutumia gharama kubwa kuhonga hata kufikia hatua ya kuuza ng'ombe.

"Mimi nimekaa kwa wamasai Monduli, nimechunga mpaka ng'ombe za wamasai nikiwa JKT Makuyuni. Ni watu wazuri tu. Sasa kwanini wamasai wa huku wanachukia mali za wengine wakulima? Nataka niwaaeleze nitalifuatilia hili.

Pamoja na hayo ameongeza "Kama yupo mmoja ambaye analiisha kila siku anajifanya ana mali huyo mimi ndiye ntalala naye mbele mwenyewe".

Mtazame hapa chini


"Huyo nitalala naye mbele mwenyewe" - JPM
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad