Kampuni inayoendesha Mradi wa Usafiri wa Mabasi ya Mwendokasi(UDART), imefungua kesi mahakamani dhidi ya Jamhuri, kupinga kitendo cha Serikali kutaka kuleta mwekezaji mpya
-
Hatua ya Serikali kutafuta mwekezaji mwingine ilitangazwa Mei 10, 2018 na Waziri Mkuu akiwa Bungeni baada ya kampuni hiyo kuonekana kusuasua katika kuendesha mradi huo
-
Itakumbukwa kuwa Kampuni ya UDART ilifunguliwa kesi ya madai Mahakamani na Kampuni ya Maxcom wiki tatu zilizopita kwa kushindwa kulipa gharama za uendeshaji, uwekezaji na hata stahiki za wafanyakazi