Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kila mtu kwa sasa anafahamu kipindi wanachopitia wao kama Yanga lakini kwa upande wake amekuwa akizungumza na wenzake ili kutambua wajibu wao kama wachezaji.
Cannavaro ameiambia Sports Xtra kuwa hakuna wachezajk waliogoma ingawa kumekuwa na maneno mengi kwa baadhi ya wapenzi wa soka nchini.
“Mimi ndio napata sana tabu kwa sababu mimi ni kiungo ambaye nawaangalia sana wachezaji wenzangu hasa katika kipindi hiki ambacho tunapita, ni kigumu sana.”
“Kila mwana Yanga anajua tunapita katika kipindi gani, lakini nawapongeza sana vijana wangu wamefanya kazi na wanastahili sifa.”
“Katika miaka yote niliyokaa Yanga, hawa vijana wanastahili sifa. Siwezi kutangaza masuala ya klabu yangu lakini vijana wanastahili sifa kwa sababu ni wastahimilivu.”
“Kuwarudisha kwenye mchezo inahitaji moyo sana unakaa na kuzungumza nao kinachosaidia ni kwamba wananisikiliza kila nikiwaambia kituna bado tunaendelea kupambama na timu yetu ili tuifikishe kwenye hali nzuri. Kwa sasa wachezaji wengi wanasumbuliwa na majeraha nikiwepo mimi mwenyewe.”
“Kwenye ligi tumekosa, sasa hivi macho yetu yapo kwenye Caf Confederation Cup kama tukiweza kupata nafasi hapa na kufika nusu fainali tunaweza kupatabupendeleo wa kuongeza timu tukapata nafasi ya kuingiza timu tatu hadi nne kwenye mashindano ya Afrika.”
“Nawaita wachezaji wazoefu tunajadili kwamba kitu fulani kina wezekana na vitu vingine haviwezekani nikimalizana na wachezaji wazoefu wale wengine vijana hawanisumbui naweza kuzungumza nao vizuri.”
“Hakuna mtu ambaue hajui Yanga imepita kwenye kipindi kigumu mwaka huu, nasikia fununu watu wanasema wachezaji wa Yanga tumegoma, hakuna mchezaji aliyegoma. Huu ni mpira wachezaji tunaendelea na mazoezi, najua kila mtanzania anajua Yanga tuna shida lakini sisi tunapambana hii ndiyo kazi yetu.”
“Sijaelewa kwa sababu kuna watu wanamaliza mikataba yao sijui viongozi watakaa vipi na wachezaji, mchezaji anapomaliza mkataba inakuwa nje ya uwezo wangu. Mtu akimaliza mkataba siwezi kuzungumza nae kwa sababu ni suala ambalo lipo nje ya mkataba wangu.”