Kenya Kutimiza Ndoto Yao ya Kisayansi Leo Kuzindua Satelaiti Katika Anga ya Juu

Kenya Kutimiza Ndoto Yao ya Kisayansi Leo Kuzindua Satelaiti Katika Anga ya Juu
Kenya inajiandaa kutimiza ndoto kubwa ya kisayansi leo Ijumaa. Chombo cha Satelaiti kilichoundwa nchini humo kitarushwa katika anga za juu hii leo kutoka nchini Japan.

Chombo hicho kilibuniwa na wanasayansi kutoka Chuo

Wanasayansi wa anga za juu kutoka Kenya waliokiunda chombo hicho tayari wako katika makao ya Uchunguzi wa Sayansi ya Anga za juu nchini Japan, (JAXA) ambapo chombo hicho kitarushwa kutoka huko.

Nchini Kenya kwenyewe raia wataweza kufuatilia shughuli hiyo moja kwa moja kwenye mtandao wa You Tube, na sherehe maalumu ya kushuhudia imeandaliwa katika chuo kikuu cha Nairobi.

Satelaiti hiyo ndogo ni ya thamani ya dola milioni moja - gharama inayoonekana kuwa ndogo kifedha kwa kiwango cha sayansi ya anga za juu.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad