Kesi ya Kina Mbowe na Wenzake yasikilizwa leo...Hicho ndio Kinaendelea


KISUTU, DAR: Kesi ya kufanya mikusanyiko isiyo halali inayowakabili viongozi 9 wa CHADEMA, imeendelea tena leo Mei 15, 2018 Mahakamani hapo
-
Katika kesi hiyo Mahakama imetupilia mbali ombi la upande wa utetezi la kutaka kesi hiyo kupelekwa Mahakama kuu
-
Hakimu anayeendesha kesi hiyo, Wilbard Mashauri amesema usikilizaji wa awali utaanza rasmi kesho Mei 16, 2018 saa nane mchana
-
Wakati kesi hiyo ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 ikisomwa leo, mshtakiwa wa 7, Halima Mdee na mshtakiwa wa 9 Ester Bulaya hawapo mahakamani
-
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala ameieleza Mahakama kuwa sababu ya washtakiwa hao kutokuwapo imetokana na usafiri waliokuwa wanatumia kutoka bungeni kuelekea Dar kuwa na tatizo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad