Wakili wa Takukuru, Leonard Swai jana amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi inayomkabili Tido leo ilipaswa kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.
Lakini shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi katika kesi hiyo ana udhuru.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Shaidi ameiahirisha kesi hiyo hadi Juni 8 ili mashahidi wa upande wa mashtaka waendelee kutoa ushahidi.
Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu wa upande wa Jamhuri wamekwishatoa ushahidi .
Mashahidi hao ni Ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.
Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.