Kigwangalla Aagiza Kuandaliwa kwa Mkataba wa Makubaliano

Kigwangalla Aagiza Kuandaliwa kwa Mkataba wa Makubaliano
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, ameagiza uandaliwe mkataba wa makubaliano ya awali (MoU) ya utekelezaji wa mradi wa kuendeleza utalii wa picha katika Pori la Akiba Selous.

Mkataba huo wa makubaliano utahusisha wawekezaji kutoka Jiji la London nchini Uingereza na Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA na utakapokamilika utasainiwa na pande zote mbili.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo akiwa ofisini kwake Jijini Dodoma kufuatia maombi yaliyowasilishwa kwake na wawekezaji hao, Eva Sanchez na Nicholas Negre.

Akiwasilisha maombi hayo, Sanchez amesema mradi huo utakuwa wa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA ambao ndiyo wasimamizi wakuu wa Pori la Akiba Selous utakapoanzishwa mradi huo.

Dk. Kigwangalla amewataka wawekezaji hao kuwasilisha andiko la mradi huo, kufanya utafiti wa kina na tathmini ya athari za kimazingira zitakazoweza kujitokeza kutokana na uanzishwaji wa mradi huo.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad